Raisi Nicolasi Maduro wa Venezuela ametangaza vyama vikuu vitatu vya nchi hiyo havitaruhusiwa kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 kutokana na vyama hivyo kususia uchaguzi wa mameya ulioafanyika jumapili.
Maduro amesema vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa Mameya siku ya jumapili ndo vitakavyoruhusiwa kusimamisha mgombea wa kiti cha uraisi mwakani.
Viongozi wakuu wa vyama vya Justice First, Popular will, na Democratic action walijitenga na uchaguzi wa mameya baada ya kulalamikia mfumo wa upigaji kura.
Kwa mujibu wa Raisi Maduro amesema vyama vya upinzani nchini humo vimepotea katika kwenye ramani ya siasa. Chama tawala chini Venezuela kimeshinda viti vya umeya 300 kati ya 335.
Venezuela: Vyama vya Upinzani vimeondolewa kutoshiriki uchaguzi 2018
Reviewed by info tza
on
1:56 AM
Rating:

No comments: