Historia ya Inspekta mkuu wa polisi tangu tupate uhuru
Nimekuwa
nikipata maswali mengi kutoka kwa wanafunzi, na watu wengine wangu wa karibu
wakiniuliza idadi ya Inspekta General (IGP) ambao tulikuwa nao tangu nchi yetu
tupate uhuru, yani Tanganyika huru na baada ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar sikuweza kuwajibu kwasababu sikuwa na jibu linalojitosheleza ikabidi
nianze kufatiia kujua.
Katika kutafuta
majibu nikawa nimefanikiwa kupata idadi yao, majina na miaka ambayo walihudumu
kabla ya kuwaachia wengine ngazi na kuendeleza kugurudumu.
Na wewe kama ni
mmoja ya watu wanaopenda kujua historia ya jeshi letu la polisi na idadi ya
wakuu wa jeshi la polisi (IGP) tangu tupate uhuru hapa nimekusogezea majina yao
na mda waliohudumu katika utumishi wa umma.
Elangwa N.Shaidi
Ni mkuu wa
kwanza kabisa wa jeshi la polisi aliyehudumu kuanzia mwaka 1964-1970 abaada ya
Muunganiko wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa jina Tanzania akiwa anahudumu
katika serikali ya awamu ya kwanza chini yake amiri jeshi mkuu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere.
Hamza Azizi
Alikuwa
akihudumu chini ya Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Julius Nyerere
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi :1970-1973
Samwel H. Pundugu
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 7/8/1973 – aug 1975
Alihudumu chini
ya Raisi Julius Kambarage Nyerere
Philemon N. Mgaya
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 8/8/1975 – Nov 1980
Alihudumu chini
ya Raisi Julius Kambarage Nyerere
Solomon Liani
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 2/11/1980 – 30/11/1984
Alihudumu chini
ya Raisi Julius Kambarage Nyerere
Harun G Mahundi
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 1/12/1984 – 3/5/1996
Alihudumu chini
ya maraisi watatu mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mheshimiwa Hassan Mwinyi,
na Mheshimiwa William Mkapa (awamu ya kwanza, pili na tatu).
Omary Maita
Omary Maita
alihudumu kama mkuu wa jeshi la polisi kuanzia tarehe 4/5/1996 hadi 2/3/2006
katika serikali ya awamu ya tatu na kidogo katika awamu ya nne ambavyo alikuwa
chini ya raisi Benjamini Mkapa na baadae akawa chini ya raisi Jakaya Mrisho kikwete
hadi hapo alipoachia ngazi mwaka 2006.
Saidi A Mwema
Alihudumu chini
ya Raisi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 3/3/2006 – 30/12/2013
Ernest Mangu 01/01/2014 – 29/05/2017
Alihudumu chini
ya maraisi wawili Jakaya Mrisho Kikwete na Mheshimiwa Dr. John Pombe Magufuli.
Simon Sirro
Muda wa kuhudumu
kama mkuu wa jeshi la polisi : 29/05/2017
– hadi sasa
Anahudumu chini
ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Magufuli.
Shirikisha na wenzako.
Listi ya inspekta wakuu wa jeshi la polisi (IGP) tangu tupate uhuru
Reviewed by info tza
on
1:57 PM
Rating:
No comments: