Hawa ndo mawaziri walioachwa nje ya baraza jipya la mawaziri
Raisi John
Magufuli amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri ikiwa ni mara yake
ya kwanza kufanya hivyo tangu aingie madarakani mwaka 2015.
Katika
mabadiliko hayo Raisi Magufuli amewaacha nje baadhi ya mawaziri waliokuwapo
katika baraza la zamani la mawaziri na kuongeza sura mpya katika baraza hilo
jipya la mawaziri.
Kati ya mawaziri
waliochwa nje ni aliyekuwa waziri wa maliasli na utalii , Profesa Jumanne
Maghembe ambaye nafasi yake imechukuliwa na Hamisi Kingwangwala aliyekuwa naibu
waziri wizara ya afya.
Pia mwingine
aliyeachwa nje ni aliyekuwa waziri wa maji na umwagiliaji, Mhandisi Gerson
Lwenge ambae nafasi yake imechukuliwa na Mhandisi Issack Kamwele
Aliyekuwa naibu
waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Annastazia Wambura naye ameachwa
nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Viti maalumu Juliana Shonza
Aliyekuwa Naibu
waziri wa maliasili na utalii Ramo Makani naye ameachwa nje na nafasi yake
kuchukuliwa na Japhet Hasunga
Mawaziri walioachwa nje ya baraza jipya la mawaziri
Reviewed by info tza
on
12:43 PM
Rating:
No comments: