Raisi wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza baraza
jipya la mawaziri leo tarehe 7/10 katika hafla fupi iiyofanyika ikulu na
kuuzuliwa na makamu wa raisi pamoja na waziri mkuu ambapo wizara zimeongezeka
kutoka wizara 19 hadi 21.
Kugawanya kwa
wizara imetokana na wizara mbili kugawanywa huku akiongeza manaibu waziri kwa
baadhi ya wizara.
Akitangaza
baraza la mawaziri Raisi Magufuli amesema wizara ya nishati na madini ambayo
ilikuwa ni wizara moja imegawanywa mara mbili, ambavyo kwa sasa kutakuwa na
Wizara ya nishati na wizara ya madini
Akizungumza
Raisi amesema lengo kubwa la kugawa wizara ya nishati na madini ni kutokana na
umuhimu wa rasilimali hiyo kwa taifa na kwamba wizara zote hizi mbili zitakuwa
na waziri na naibu wake.
Raisi ametaja
mabadiliko mengine katika wizara ya kilimo, mifugo, na uvuvi ambavyo kwa sasa
kutakuwa na wizara ya kilimo inayojitegemea na wizara nyingine itakuwa ni
wizara ya mifugo na uvuvi.
Akiongea Ikulu
Raisi Magufuli amesema sababu ya kufanya mabadiliko katika wizara ya kilimo,
mifugo na uvivu kuwa wizara mbili tofauti ni kutokana na umuhimu wa sekta hii
muhimu inayoajiri asilimia kubwa ya watanzania zaidi ya asilimia 75, kila
wizara itakuwa na waziri na naibu waziri wake.
Mabadiliko
mengine ni katika wizara ya Tamisemi baada ya kuwekewa manaibu waziri kwasababu
ni wizara inayogusa sehemu kubwa ya wananchi.
Pia katika
wizara ya Viwanda na biashara ameiongezea naibu waziri ili kuharakisha shughuli
za kimaendelea tofauti na hapo mwanzo ambapo ilikuwa na waziri pekee.
Orodha ya mawaziri hii hapa
- Wizara ya Ofisi ya Raisi Utumishi na Utawala bora
Waziri ----
George Huruma Mkuchika
- Wizara ya TAMISEMI
Waziri
------ Suleiman Japho
- Wizara ya Mifugo na Uvuvi
Waziri
------ Luhaga Mpina
Naibu Waziri
----- Abdallah Ulega
- Wizara ya Maji na umwagiliaji
Waziri – Isack Kamwelwe
Naibu waziri –
Juma Hamidu Aweso
- Wizara ya habari, utamaduni, wasanii na michezo
Waziri – Dr.
Harrison Mwakyembe
Naibu waziri –
Juliana Shonza
- Wizara ya afya, maendeleao ya jamii, jinsia, wazee na watoto
Waziri – Ummy Mwalimu
Naibu waziri – Faustine
Ndugulile
- Wizara ya Elimu, sayansi, Teknolojia na Ufundi
Waziri – Joyce Ndalichako
Naibu waziri –
William Ole Nasha
- Wizara ya viwanda, biashara, na uwekezaji
Waziri – Charles
Mwijage
Naibu waziri –
Stella Manyanya
- Wizara ya Maliasili na utalii
Waziri – Hamisi Kinwangala
Naibu waziri –
Ngailonga Josephat
- Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi
Wizara – William
Lukuvi
Naibu waziri –
Angelina Mabula
- Wizara ya mambo ya ndani
Waziri – Mwigulu
Nchemba
Naibu waziri –
Hamad Masauni
- Wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga taifa
Waziri – Dr. Hussein
Mwinyi
- Wizara ya katiba na Sheria
Waziri –
Palamagamba Kabudi
- Waziri wa mambo ya nje, ushirikiano wa afrika mashariki, kikanda na kimataifa
Waziri –
Agustino Mahiga
Naibu waziri –
Dkt Susan Kolimba
- Wizara ya madini
Waziri – Angela Kairuki
Naibu waziri –
Haroon Nyongo
- Wizara ya nishati
Waziri – Medrad Matogoro
Kalemani
Naibu waziri –
Subira Hamisi Mgalu
- Wizara ya Fedha na mipango
Waziri – Dr Philip
Mpango
Naibu waziri –
Dr Ashatu Kijaji
- Wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano
Waziri – Prof.
Makame Mbarawa
Naibu waziri –
Atashasta Nditiye
Naibu waziri –
Eliasi John Kwandikwa
- Wizara ya kilimo
Waziri – Charles
John Tizeba
Naibu waziri –
Mary Mwanjelwa
- Wizara ya Waziri mkuu: Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu
Waziri – Jenista
Mhagama
Naibu waziri –
Anthony Peter Mavunde
Naibu waziri
walemavu – Stela Alex Likupa
- Wizara ya ofisi ya makamu wa raisi, muungano na mazingira
Waziri – January
Makamba
Naibu Waziri –
Kangi Lugola
TANZANIA: Raisi Magufuli atangaza baraza Jipya la Mawaziri
Reviewed by info tza
on
12:15 PM
Rating:

No comments: