Nchi zenye nguvu za kijeshi duniani
Kwa mujibu wa mtandao wa powerrank huwa wanatoa listi
ya nchi zenye nguvu za kijeshi duniani kila mwaka.
Hivi na baadhi ya vigezo wanavyovitumia kutoa safu ya
nchi zenye nguvu za jeshi duniani.
- Wastani wa idadi ya watu ikiwemo wenye nguvu ya kufanya kazi, idadi ya walio na uwezo wa kujiunga na jeshi na walio mstari wa mbele vitani na idadi ya waliobaki kama akiba ikiwa wameingia vitani.
- Idadi ya mizinga na magari yaliyojihami kupigana.
- Manuari yenye kituo cha ndege za kushambulia, nyambizi za chini ya maji ndege zenye uwezo wa kuepusha mashambulizi, na helkopita.
- Pia wanaangalia uwezo wa jeshi kusambaza vifaa kama malazi, vifaa vya jeshi kwa jeshi lake, teknolojia inayotumiwa na jeshi,
- Bajeti ya ulinzi na usalama kwa nchi husika na uwezo wake wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi. Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Pia katika kupanga safu pia nchi ndogo kieneo na yenye
idadi ndogo ya watu ila ina uwezo mkubwa wa kiitelijensia zinapabanishwa na
nchi kubwa kieneo lakini haina
intelijensia nzuri, ila inanyimwa nguvu kutokana na kutokuwa na uwezo wa
kulinda pwani ya nchi.
Marekani.
Marekani ni nchi ya kwanza duniani yenye nguvu za
kijeshi duniani kutokana na uwekezaji mkubwa katika bajeti yake ikiwa ni zaidi
ya $612.5 bilioni. Ina jumla ya idadi ya wanajeshi milioni 1.4 waliotiyari
kuingia vitani ikiwa nchi imevamiwa na ziada ya wanajeshi 8,000,000 kama akiba,
ikiwa watahitajika mda wowote wanakuwa wapo tiyari.
Marekani ni kati ya nchi chache duniani yenye
teknolojia kubwa sana ya jeshi, ikiwa na silaha hatari sana kama silaha za
nyuklia vipatavyo vichwa 7500 pamoja na manowari za kijeshi na nyambizi za
majini.
Urusi
Nchi ya Urusi inafatia kuwa na nchi ya pili yenye nguvu
duniani, kabla ya umoja wa kisovieti kuvunjika nan chi za ulaya mashariki
kujitenga kutoka umoja huo nguvu za nchi hiyo zilipungua ukilinganisha na
marekani. Bajeti yake kwa mwaka ni dola za kimarekani $76.6 bilioni ikitegemewa
bajeti hiyo itaongezwa zaidi ya asilimia 44 kwa miaka mitatu ijayo. Inayo zaidi
ya wanajeshi 766,000 mstari wa mbele vitani na wanajeshi milioni 2.5 wakiwa
wamewekwa kama akiba na vifaru 15,500 ikiwa nd nchi kubwa yenye nguvu ya vifaru
duniani, ikiwa na vichwa vya nyuklia pia.
China
China ni nchi iliyopakana na nchi kama Korea Kaskazini,
Korea kusini, Japani, etc. pia china ina nguvu kubwa za kiuchumi ukilinganisha
na Russia na inakimbiza ikiwa na uchumi unaokua kwa kasi sana duniani.
Bajeti yake kwa mwaka ni dola za Marekani $216 bilioni,
ikiwa na wanajeshi milioni 2.29 walio mstari wa mbele vitani na ziada ya
wanajeshi milioni 2.3 waliowekwa kama akiba. Ina zaidi ya magari ya 25,000.
India
India ni nchi ya nne yenye nguvu kijeshi duniani yenye
bajeti ya dola bilioni 40.4. Jeshi la nchi lina jumla ya wanajeshi milioni 3.5
ikiwa na milioni 1.3 wakiwa tiyari kwa vita. Ina jumla ya magari 16,000 ya nchi
kavu, nguvu za anga zaidi ya ndege na helkopita kwa jumla yake ni 1,785, ikiwa
na vichwa vya nyuklia pia.
Uingereza
Ni kati ya nchi zenye nguvu barani Ulaya ikiwa bajeti
ya ulinzi na usalama ni dola bilioni 54. Idadi ya wanajeshi 205,000, na ndege
ndogo za kivita 908 na manuari 66 za kivita.
France
Nchi ya ufaransa inatumia asilimia 1.9 ya GDP yake kama
bajeti ya ulinzi na usalama wan chi ikiwa ni dola biioni 43. Ina wanajeshi
milioni 5 ikiwa na wanajeshi milioni 2.2 walio tiyari kuingia vitani na ziada
ya wanajeshi 2.8 milioni kama akiba. Magari ya nchi kavu ni 9000 na nguvu za
anga wakiwa na ndege 1,000 za kivita zikiwemo na helkopita.
Ujerumani
Ni nchi yenye uchumim mkubwa ukilinganisha nan chi
nyingine barani Ulaya. Bajeti yake kwa mwaka ni dola bilioni 32.9. wanajeshi
milioni 1.83 wapo mstari wa mbele kuingia vitani endapo ikitokea kwa sasa na
ziada ya wanajeshi milioni 1.45 kama akiba.
Nchi zenye nguvu za kijeshi duniani
Reviewed by info tza
on
12:23 PM
Rating:
No comments: