Tovuti ya Global fire.com kila mwaka inatoa safu ya
jeshi duniani kutokana na ubora wake wa kijeshi unaotokana na ubora wa jeshi
katika nchi husika. Safu ya utofauti wa kijeshi kwa nchi za kiafrika zenye
nguvu za kijeshi na kivita zimetajwa mwaka huu.
Katika kuandaa safu ya nchi yenye nguvu wanahusisha
vigezo vifuatavyo: wastani wa idadi ya watu walio mstari wa mbele vitani na
idadi ya waliobaki kama akiba ikiwa wameingia vitani. Idadi ya mizinga na
magari yaliyojihami kupigana. Manuari yenye kituo cha ndege za kushambulia,
ndege zenye uwezo wa kuepusha mashambulizi, na helkopita.
Pia wanaangalia uwezo
wa jeshi kusambaza vifaa kama malazi, vifaa vya jeshi kwa jeshi lake, teknolojia
inayotumiwa na jeshi, bajeti ya ulinzi na usalama kwa nchi husika na uwezo wake
wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi.
Katika kupanga safu pia nchi ndogo kieneo na yenye
idadi ndogo ya watu ila ina uwezo mkubwa wa kiitelijensia zinapabanishwa na
nchi kubwa kieneo lakini haina
intelijensia nzuri, tatizo kubwa la nchi ndogo kuweza kuwekwa safu ya kwanza
licha ya intelijensia yake kuwa nzuri ni uwezo wake mdogo wa kuweza kulinda
pwani yake kutokana na kutokuwa na uwezo wa manuari za kijeshi endapo
ikishambuliwa kutokea majini.
Pia wanaangalia uwezo wan chi kulipa deni lake ikiwa
inadaiwa, uwezo wake wa ubadirshaji wa fedha za kigeni au dhahabu.
Kutokana na vigezo hivi nimekusogezea nchi kumi zenye
uwezo mkubwa wa kijeshi barani afrika.
Nchi yenye jeshi imara africa
- Misri
Misri ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana
kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi
kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali
asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $4.4 kwa
mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara
mengine kwa ujumla
Misri ina wastani ya watu wapatao 94,666,993, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 35,306,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 1,535,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 1,329, 250. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla
wakiwa ni wanajeshi 454,250 na wanajeshi 875,000 wakiwa wamewekwa kama akiba
endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya
ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 1,132.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi
ikiwa idadi yake jumla ni 22,080.
Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa
kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye
kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari
pamoja na nyambizi za jeshi zipatazo tano. Kwa ulinzi wa majini nchi ya misri
ina jumla ya silaha 319.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya misri ina uwezo wa kuzalisha mapipa 478,400 kwa
siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 740,000 kwa siku. Huku ikiwa
na akiba ya mapipa 4,400,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya misri ina bandari 7, zaidi ya kilomita 65,050 za
barabara, kilomita 5,083 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 83.
- Algeria
Algeria ni nyingine barani afrika iliyoendelea sana
kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi
kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali
asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $10.6 kwa
mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara
mengine kwa ujumla.
Algeria ina wastani ya watu wapatao 40,263,711, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 20,400,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 675,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 792,350. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa
ni wanajeshi 520,000 na wanajeshi 272,350 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo
wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya
ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 502 ikiwa ni ndogo
kulinganisha na nchi kama Misri.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi
ikiwa idadi yake jumla ni 9,825.
Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa
kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye
kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari
pamoja na nyambizi za jeshi zipatazo sita. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Algeria
ina jumla ya silaha 85.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Algeria ina uwezo wa kuzalisha mapipa 1,370,000
kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 350,000 kwa siku. Huku
ikiwa na akiba ya mapipa 12,000,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya Algeria ina bandari 9, zaidi ya kilomita 111,261 za
barabara, kilomita 3,973 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao
157.
- Ethiopia
Ethiopia ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea
sana kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana
kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa
rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola milioni
$340 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na
mabara mengine kwa ujumla
Ethiopia ina wastani ya watu wapatao 102,374,044, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 40,000,000 na waliofikisha umri wa kujiunga
na jeshi 1,950,000 , jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao
162,000. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni
wanajeshi 162,000 na wakiwa hawana wanajeshi wa akiba.
Wana uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya
ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 80.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi
ikiwa idadi yake jumla ni 2,568.
Hawana manuari na nyambizi za jeshi kutokana na jiografia
ya nchi yao.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Ethiopia ina uwezo wa kuzalisha mapipa 100 kwa
siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 57,000 kwa siku. Huku ikiwa
na akiba ya mapipa 430,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya Ethiopia ina bandari 2, zaidi ya kilomita 36,469 za
barabara, kilomita 681 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 57.
- Nigeria
Nigeria ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea
sana kijeshi licha ya changamoto za ugaidi kwa kigundi cha itikadi kali ya
kiislamu Boko Haramu ambacho kimekuwa na tabia ya kuteka na kuuua wananchi
ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana
na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama
mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $2.33 kwa mwaka ikiwa
kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla.
Nigeria ina wastani ya watu wapatao 186,053,386, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 72,400,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 3,456,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 181,000. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa
ni wanajeshi 124,000 na wanajeshi 57,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo
wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Uwezo wake wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya ndege
za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za usafirishaji,
helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 110.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi
ikiwa idadi yake jumla ni 1962.
Uwezo kuweza
kupigana vita vya majini kwa kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya
diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa
kushambulia na kurudi kwenye manuari, wakiwa hawana nyambizi. Kwa ulinzi wa
majini nchi ya Nigeria ina jumla ya silaha 75.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Nigeria ina uwezo wa kuzalisha mapipa 2,423,000
kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 302,000 kwa siku. Huku
ikiwa na akiba ya mapipa 37,000,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya misri ina bandari 3, zaidi ya kilomita 193,200 za
barabara, kilomita 3,505 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 54.
- Afrika kusini
Afrika kusini ni nchi mojawapo barani afrika
iliyoendelea sana kijeshi na yenye uchumi mzuri ikiwa na silaha nyingi za
kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu
walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku
bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $4.61 kwa mwaka ikiwa kubwa sana
ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara mengine kwa ujumla
Afrika kusini ina wastani ya watu wapatao 54,300,704,
huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 26,000,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 965,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 94,050.
Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa
ni wanajeshi 78,050 na wanajeshi 16,000
wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na
kupigana.
Wan uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya
ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 231.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi
ikiwa idadi yake jumla ni 2650.
Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa
kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye
kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari pamoja
na nyambizi za jeshi zipatazo tatu. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Afrika kusini
ina jumla ya silaha 30.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Afrika kusini ina uwezo wa kuzalisha mapipa
3000 kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 605,000 kwa siku.
Huku ikiwa na akiba ya mapipa 15,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya Afrika kusini ina bandari 5, zaidi ya kilomita
362,099 za barabara, kilomita 20,192 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege
vipatao 566.
- Angola
Angola ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana
kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi
kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali
asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $4.2 kwa
mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara
mengine kwa ujumla
Angola ina wastani ya watu wapatao 20,172,332, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 6,030,000 na waliofikisha umri wa kujiunga
na jeshi 310,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao
175500. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni
wanajeshi 107,000 na wanajeshi 68,500 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo
wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Wana uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla ya
ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 285.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 1,257.
Uwezo mkubwa kuweza kupigana vita vya majini kwa
kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye
kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari,
hawana nyambizi za kivita. Kwa ulinzi majini nchi ya Angola jumla ya silaha 57.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Angola ina uwezo wa kuzalisha mapipa 1,742,000
kwa siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 133,000 kwa siku. Huku
ikiwa na akiba ya mapipa 8,400,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ya Angola ina bandari 4, zaidi ya kilomita 51,429 za
barabara, kilomita 2,764 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao
176.
- Morocco
Morocco ni nchi nyingine barani afrika iliyoendelea
sana kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana
kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa
rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni
$3.4 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na
mabara mengine kwa ujumla
Morocco ina wastani ya watu wapatao 33,655,786, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 17,000,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 600,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 373,000.
Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa
ni wanajeshi 198,000 na wanajeshi 175,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo
wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Morocco pia ina uwezo mkubwa wa ulinzi wa anga wakiwa
na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 278.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 4,336.
Uwezo mkubwa wa kuweza kupigana vita vya majini kwa
kutumia manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye
kubeba ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari
haina nyambizi. Kwa ulinzi wa majini nchi ya morocco ina jumla ya silaha 121.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya morocco ina uwezo wa kuzalisha mapipa 500 kwa
siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 210,000 kwa siku. Huku ikiwa
na akiba ya mapipa 680,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ina bandari 5, zaidi ya kilomita 58,395 za barabara,
kilomita 2,067 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 55.
- Sudan
Sudan ni nchi mojawapo barani afrika iliyoendelea sana
kijeshi ikiwa na silaha nyingi za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana kijeshi
kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa rasilimali
asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola bilioni $2.5 kwa
mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika na mabara
mengine kwa ujumla
Sudan ina wastani ya watu wapatao 36,729,501, huku
wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 20,850,000 na waliofikisha umri wa
kujiunga na jeshi 1,045,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi
wapatao 282,150. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa
ni wanajeshi 171,150 na wanajeshi 105,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo
wakihitajika jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Sudani pia wana uwezo wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla
ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 181.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo
vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 1,566.
Uwezo wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia
manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba
ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari wakiwa
hawana nyambizi. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Sudani ina jumla ya silaha 18.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Sudan ina uwezo wa kuzalisha mapipa 64,770 kwa
siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 94,500 kwa siku. Huku ikiwa
na akiba ya mapipa 5,000,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa kusafirisha
watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mda wote wa
vita. Nchi ina bandari kuu 1, zaidi ya kilomita 11,900 za barabara, kilomita
5,978 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao 74.
- Libya
Libya ni nchi iliyokumbwa na matatizo makubwa ya
kiusalama baada ya kuuliwa kwa raisi wake wa mda mrefu kanali Gaddafi iiyopo
barani afrika iliyoendelea kijeshi ikiwa na silaha za kivita na uwezo mkubwa wa
kupambana kijeshi kutokana na idadi ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa
wa rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola
bilioni $3.0 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika
na mabara mengine kwa ujumla
Libya ina wastani ya watu wapatao 6,541,948, huku wenye
nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 3,500,000 na waliofikisha umri wa kujiunga na
jeshi 117,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na idadi ya wanajeshi wapatao 100,000.
Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea vita ghafla wakiwa ni wanajeshi
35,000 na wanajeshi 65,000 wakiwa wamewekwa kama akiba endapo wakihitajika
jeshini wako tiyari kuenda na kupigana.
Libya pia wana uwezo wa ulinzi wa anga wakiwa na jumla
ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za kushambulia, ndege za
usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa ni 121.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha zikiwemo
vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 1,399.
Uwezo wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia
manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba
ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari wakiwa
hawana nyambizi. Kwa ulinzi wa majini nchi ya Libya ina jumla ya silaha 5.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ya Libya ina uwezo wa kuzalisha mapipa 470,000 kwa
siku. Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 250,000 kwa siku. Huku ikiwa
na akiba ya mapipa 48,360,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ina bandari kuu 4, zaidi ya kilomita 100,024 za
barabara, kilomita 2,757 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao
146.
- Jamhuri ya watu wa kongo
Jamhuri ya watu wa kongo ni nchi mojawapo barani afrika
iliyoendelea kijeshi ikiwa na silaha za kivita na uwezo mkubwa wa kupambana
kijeshi kutokana na idadi kubwa ya watu walio nao na kuwa na uwezo mkubwa wa
rasilimali asilia kama mafuta na gesi huku bajeti yake ya jeshi ni dola milioni
$162 kwa mwaka ikiwa kubwa sana ukilinganisha na mataifa mengine Afrika.
Jamhuri ya watu wa kongo ina wastani ya watu wapatao
81,331,050, huku wenye nguvu ya uzalishaji wakiwa watu 16,000,000 na
waliofikisha umri wa kujiunga na jeshi 1,750,000, jeshi la nchi hiyo likiwa na
idadi ya wanajeshi wapatao 144,625. Waliotiyari kuingia vitani endapo ikitokea
vita ghafla wakiwa ni wanajeshi 144,625 na hawana wanajeshi wa akiba
Jamhuri ya watu wa kongo pia wana uwezo wa ulinzi wa
anga wakiwa na jumla ya ndege za kivita zikiwemo helkopita, ndege za
kushambulia, ndege za usafirishaji, helkopita za ushambuliaji idadi yake ikiwa
ni 41.
Katika ulinzi wa ardhini (kupigana vita vya ardhini)
wakiwa vizuri sana kijeshi pia kutokana na kuwa na idadi kubwa ya silaha
zikiwemo vifaru, magari ya jeshi, roketi ikiwa idadi yake jumla ni 510.
Uwezo wa kuweza kupigana vita vya majini kwa kutumia
manuari za kivita zinazotumia mafuta ya diseli, umeme na nyuklia, zenye kubeba
ndege za kivita zenye uwezo wa kushambulia na kurudi kwenye manuari wakiwa
hawana nyambizi. Kwa ulinzi wa majini nchi ina silaha 1.
Kutokana na wingi wa silaha nyingi za kijeshi duniani
unategemea sana upatikanaji wa rasilimali asilia kama mafuta ya petrol
inayopimwa kwa kuangalia uzalishaji wa idadi ya mapipa kwa siku.
Nchi ina uwezo wa kuzalisha mapipa 20,000 kwa siku.
Huku matumizi yake kama nchi ikiwa ni mapipa 9,320 kwa siku. Huku ikiwa na
akiba ya mapipa 180,000,000.
Nchi haiwezi kupigana vita hasa kama haina uwezo wa
kusafirisha watu na vifaa vya jeshi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine
mda wote wa vita. Nchi ina bandari kuu 11, zaidi ya kilomita 153,497 za
barabara, kilomita 4,007 za reli na vituo vya kuruka na kutua ndege vipatao
198.
Nchi yenye jeshi imara afrika
Reviewed by info tza
on
12:07 PM
Rating:
No comments: