Kujali afya yako kipindi cha ujauzito ni muhimu sana.
Mwili wako utakuwa unahitaji zaidi virutubisho, vitamin na madini joto
mbalimbali mwilini mwako.
Chakula kikikosa virutubisho muhimu inaweza kuathiri
maendelea ya mtoto. Kikawaida unahitaji karoli 350-500 kwa siku au zaidi.
Ulaji hafifu na unene kuzidi kiasi utakuongezea hatari
ya kisukari au matatizo mda wa kujifungua.
Uchaguzi mzuri wa mlo kipindi cha ujauzito itakusaidia
kujihakikishia afya yako na mtoto na itakuwa rahisi sana kwako kupunguza unene
baada ya kujifungua.
Hapa nimekusogezea vyakula unavyopaswa kula ukiwa na
mimba (mama mjamzito)
- Viazi vitamu
Viazi vitamu vina mchanganyiko wa karotini ambayo
inabadilishwa kuwa vitamin A kwenye mwili wa binadamu.
Kazi ya vitamin A inasaidia sana kwenye ukuaji na
utofautishaji wa seli na tissue (mkusanyiko wa seli mwilini) .
Mama mjamzito anashauriwa kuongeza vitamin A mwilini
kwa zaidi ya chini ya aslimia 40 mpaka 45.
Hapaswi kutumia vitamin A inayotokana na wanyama ambayo
akila sana inaweza ikamsababishia sumu mwilini.
Pia viazi vitamu vina nyuzi nyuzi ambayo inasaidia
kupunguza kiasi cha sukari na kuboresha afya ya mfumo wa mmengenyo wa chakula.
- Mayai
Mayai yana karibia kila kirutubisho kinachoitajiwa na
mama mjamzito. Mayai makubwa yana karoli 90, protini na fat pia. Yana vitamin
na madini pia.
Mayai ni kizarishaji kizuri cha kolini (choline) ambayo
inasaidia kwenye kuboresha afya na ubongo wa mtoto. Yai moja lina zaidi ya mg
113 ya choline ambayo ni sawa na asilimia 25 kwa matumizi ya kila siku
yaliyoshauriwa ba daktari.
- Parachichi
Maparachichi yana nyuzi, vitamini B, K, E, C na copper.
Parachichi inashauliwa kutumiwa na mama mjamzito kwa kuwa inasaidia kuboresha
mwili, akili na tishu (mkusanyiko wa seli mwilini) za kiumbe kilichopo tumboni.
Inaweza ikasaidia pia kuzuia kuathiriwa kwa neva.
- Maji
Wakati wa ujauzito ujazo wa damu unaongezeka kwa zaidi
ya lita 1.5, kwahiyo unashauriwa uwe/ukae na maji ya kutosha mwilini mwako. Hii
ni kutokana na kijusi kikihitaji kila kitu inabidi kipate kwa wakati,
usipofatilia afya yako ya maji unaweza kukumbwa na upungufu mkubwa w maji
mwilini mwako.
Maji yakipungua mwilini mwako utahisi kichwa kinauma,
mshutuko, uchovu, kutojihisi vizuri na kufanya usahau sahau.
Pia unywaji wa maji utakusaidia kuondoa tatizo la
maambukizo ya mfumo wa mkojo ambalo linawakumba wanawake wengi kipindi cha
ujauzito.
Unashauriwa kunywa lita 1 hadi 2 za maji kila siku, pia
unaweza kupata maji kutoka kwenye matunda na chai pia. Kila unachokula kipindi cha ujauzito kinaongeza au
kuharibu nguvu za mtoto.
- Mtama
Mtama una nyuzi nyuzi nyingi na virutubisho vingi
ikiwemo vitamin E, Selenium na plant phytonutrients (ni mchanganyiko wa mimea
unaolinda seli).
- Maharage
Maharage yana protini na pia yana nyuzi nyuzi. Ukiwa na
mimba unakuwa katika hatari kubwa ya kupata maumivu makali sana. Nyuzi nyuzi
zitasaidia kuondoa ilo tatizo. Kwa misingi hiyo bhasi jitahidi kufanya maharage
yawe chakula chako cha kila siku.
Maharage pia yanazalisha madini yakiwemo zinki ambayo
yanasaidia katika makuzi ya kiumbe kilichopo tumboni.
- Mbonga mbonga zenye rangi
Kula mbogamboga na matunda yenye rangi nyekundu,
kijani, chungwa, na nyeupe itasaidia wewe na mtoto wako kupata virutubisho.
Kila rangi ya mbogamboga au tunda inaongeza vitamin na madini tofauti mwilini
mwako.
Ukimwezesha mtoto kwa kula matunda na mbogamboga akiwa
tumboni unamsaidia mtoto kutambua ladha yake na kumsaidia kula hapo baadae
akishazaliwa.
Vyakula vya mama mjamzito
Reviewed by info tza
on
2:24 PM
Rating:
No comments: