Korea kusini kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini 2017


Korea kusini kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje amesema wataiwekea vikwazo zaidi Korea Kaskazini kutokana na tabia yake ya kutengeneza na kurusha makombora ya kinyuklia. 

Korea Kaskazini ambayo hadi desemba mwaka wamefanyia majaribio zaidi ya makombora 7 ya kinyuklia yanayoonekana kuwa hatari sana na kuhatarisha nchi majirani zake kama Japan, Korea kusini. 

Jaribio la hivi karibuni ambalo lina uwezo wa kupiga bara moja hadi jingine limeonekana kuwa hatari zaidi na kuitisha nchi ya Marekani, hali iliyomfanya raisi wa Marekani Donald Trump kutoa wito kwa mataifa duniani kuitenga Korea Kaskazini. Kauli yake hiyo imeonekana kupingwa na nchi ya Urusi kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje akidai Marekani ndo wanaoichokoza Korea Kaskazini. 

Kutazama video 



Korea kusini kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini 2017 Korea kusini kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini 2017 Reviewed by info tza on 2:42 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.