Binadamu wote wanaume kwa wanawake wa rangi zote weusi,
weupe, kabila na dini zote hakuna anayependa aonekane mzee kabla ya umri wake,
ila tabia ya kujirusha bila njia sahihi ndo itakufanya uonekane hivyo.
Ukiwa na mfumo mbaya wa maisha haimanishi umaskini
hapana. Umaskini huwezi kufanya mtu azeeke ila atazeeka kutokana yeye
anauchukuliaje huo umaskini. Kiasi kikubwa watu wanaonekana wazee kabla ya umri
wao kutokana mfumo usiyo sahihi (mbaya) wa maisha unaoweza kukusababishia
matatizo ya kiafya ikiwemo kuwa na tumbo nene sana(Kitambi), ugonjwa wa
kisukari na kadhalika.
Ukitazama ngozi inakuwa nyembamba na imekauka hii
itakusababishia michirizi kwenye ngozi yako na makunyazi pia usoni.
Mazingira, mfumo wako wa maisha, mfumo wako wa kula
inaweza kukusababishia uonekane ujihisi mkubwa na mzee pia.
Ili kuweza kuweka ngozi yako imara itakubidi kujiepusha
na mifumo Fulani ya maisha unayoyaishi kwa sasa ili uweze kufanikiwa hii
itakusaidia sana kuboresha ngozi yako haraka sana.
Kutokana na tatizo hili kuwakumba watu wengi nami
nikiwa miongoni mwao. Nimejitahidi kufatalia kujua kwanini watu wengi tunazeeka
mapema kabla ya umri wetu. Hizi hapa ni baadhi ya majibu niliyoyapata.
Imenibidi kukushirikisha na wewe ili tubadili mifumo yetu ya maisha.
Hizi ni baadhi ya tabia zitakazokufanya uonekane mzee
Uvutaji
Uvutaji haimanishi lazima uwe wewe ndo unavuta hapana,
ila ukiwa unatumia mda wako mwingi ukiwa na marafiki, ndugu na jamaa wanaovuta
sigara basi tambua na wewe upo kwenye hatari ya kuharibu ngozi yako.
Kumbuka uvutaji wa sigara, shisha au kitu chochote kile
kunaharibu afya yako kwa njia mbalimbali ikiwemo.
Kuharibu inni, hii ni kutokana na madawa yaliyopo
kwenye sigara yanaweza kukusababishia madhara ya kupumua (Unapumua kwa shida)
hii ni kutokana na kuharibu cell za ngozi hewa ya oksijeni (O2)
kupita.
Kunywa kupita kiasi (Excess drinking)
Pombe yoyote ile ni kilevi tosha, ukinywa kupita kiasi
itakusababishia upunguaji wa maji asili ya mwili ambayo itakufanya uonekane
mzee kabla ya umri wako. Pia unywaji wa pombe kupitiliza utakusababishia
upoteze virutubisho vya afya ya mwili wako ikiwemo vitamin A na C,
vinavyosaidia ngozi yako iwe na afya mda wote.
- Jiadhari na asira(Tunza asira yako)
Mara nyingi naamini watu wengi tunaamini sana katika
msamaha (kusamehe mwenzako ikiwa amekukosea). Kutunza asila ikiwa Fulani
amekuudhi au kuna hali Fulani huipendi kutoka kwake sio vizuri kwa afya yako na
mwonekano wako.
Kama haupo tiyari kusamehe unaongoza mawazo katika
maisha yako amabayo itakusababishia uongezaji wa hormoni inayoitwa Cortisol
itakayokupelekea kukuongezea uzito, msukumo wa damu na kisukari.
Jaribu kusamehe hata kwa kujaribu tu itakusaidia kukaa
salama kiakili na mwili pia.
Kutolala mda wa kutosha
Watu wengi siku hizi kutokana na hali ya maisha ilivyo,
wengi wetu tunajikuta tunalala mda umeenda sana na kasha kuamka mapema
kuendelea na shughuli za kutuongezea kipato. Na mda mwingi ukiwa umelala
utapata usingizi mangamumangamu utakaokufanya uonekane umechoka kweli kweli.
Ili uweze kuwa na ngozi nzuri jitahidi kutoa kipaumbele
kwa usingizi, lala kati ya masaa 7 hadi 9 kwa siku. Ila epuka kulala sana pia inaweza ikakusababishia
makunyanzi usoni.
Mawazo
Kila binadamu ana mawazo , na hali ya maisha ikiwa
mbaya inafanya watu wengi wapate msongo wa mawazo mda wote anawaza kuhusu
maisha, jinsi atakavyojiongezea kipato, matunzo ya familia, kusomesha watoto na
mengineo. Ni bora kupunguza mawazo kama unataka uwe na ngozi nzuri.
Kutojali ngozi yako
Kutojali ngozi yako ya mwili pia itakusababishia
uonekane mzee. Ili uweze kujali ngozi yako jitahidi uoshe uso wako mara mbili
kwa siku na baada yay a mazoezi au
ukitoa tu jasho nawa kwa maji safi kasha pangusa kwa kutumia kitambaa/taulo
safi na salama. Hii itakusaidia kuondoa uchafu na make up kwa wadada.
Pia kwa wadada na wamama jitahidi kunawa make up yako
kabla hujaenda kulala. Kemikali zilizopo kwenye make up zinaweza kuharibu
vinyweleo vya ngozi yako. Hakikisha ugusi usoni pako hasa sehemu muhimu kama
jicho.
Hitimisho:
Ubora wa ngozi yako ni muhimu sana itakusaidia kukuepusha na magonjwa mbalimbali ya ngozi huku ukionekana maridadi. Kama umependa maelezo haya washirikishe na wenzako, kama una tatizo, wazo au swali andika kwenye comment box utajibiwa.
Tabia zitakazokufanya uonekane mzee haraka nje ya umri wako
Reviewed by info tza
on
1:47 PM
Rating:
Iko poa
ReplyDelete