Nchi tajiri duniani 2017
Kuweza kutambua kwamba nchi Fulani ni tajiri au
masikini, unahitaji kufahamu kwanza pato la taifa kwa rasilimali yenye thamani
bayana .
Nini maana ya GDP (Pato la taifa)
Pato la taifa linapimwa kwa kuangalia thamani ya bidhaa
nzuri zilizofungwa kabla ya kuuzwa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kwa
mwaka husika ambayo hubadilishwa kuingia kwenye soko ambalo kwa sasa
linathibitiwa na pesa za kimarekani (dollar), unagawanya kwa wastani wa wingi
wa watu kwa kila nusu mwaka katika mwaka husika.
Kwahiyo kuweza kutambua nchi Fulani ni tajiri inabidi
utumie data za mwaka uliopita mfano kwa mwaka huu 2017, kuweza kujua nchi
tajiri duniani utatumia data za mwaka uliopita. Na hapa nimekusogezea nchi kumi
tajiri duniani kwa mwaka 2017 kutokana na benki kuu ya dunia.
Luxembourg - $101,994
Ni nchi ndogo sana ya bara la Ulaya iliyozungukwa nan
chi kama Ufaransa, Ubelgiji, na Ujerumani. Uchumi wa Luxembourg unategemea
zaidi biashara za kibenki, viwanda na biashara ya chuma cha pua. Wastani wa
watu kwa mwaka 2013 ulikuwa watu L 5.4 ikiwa na GDP ya 60.1 Bilioni dola za
Marekani.
Switzerland - $80,675
Ni nchi ya katikati mwa bara Ulaya yenye uchumi imara
sana, mito na miinuko mikubwa ya Alps. Uchumi wake umeegemea zaidi kwenye
uchumi wa kibenki na utengenezaji wa fedha. Kwa mwaka 2013 ilikuwa na watu 8.1
milioni, ikiwa na GDP 685.4 Bilioni dola za kimarekani.
Qatar - $76,576
Ni nchi kijangwa ya kiarabu iliyopo mashariki ya kati
bara Asia. Uchumi wake unategemea sana mauzo ya mafuta na gesi asilia. Kwa
mwaka 2013 ilikuwa na idadi ya wastani wa watu wapatao 2.169 milioni, ikiwa na
GDP ya 203.2 bilioni fedha za marekani.
Norway - $74,822
Ni nchi ya Scandinavia yenye milima, eneo lake kubwa
likiwa ni la kijani na makumbusho. Uchumi wa Norway ulikuwa unategemea sana
uvuvi wa samaki ila ulianza kukua kwa kasi baada ya kuanzisha viwanda nchini
humo. Kwa sasa uchumi wake ni uchumi mchanganyiko unaomilikiwa na serikali.
Idadi ya watu kwa mwaka 2013 ilikuwa 5.084 milioni ikiwa na GDP ya 512.6
bilioni kwa fedha za marekani.
United States - $55,805
Ni nchi ya Amerika Kaskazini ikiwa imezungukwa na
Alaska upande wa kaskazini magharibi na Hawaii upande wa bahari ya Pasifiki. Ni
mzalishaji mkubwa wa mafuta na gesi pia ni nchi kuwa ya kibiashara duniani.
Idadi ya watu kwa mwaka 2013 ni 316.5 milioni na ikiwa na GDP ya 16.77 trilioni
kwa fedha za marekani.
Singapore - $52,888
Singapore ni nchi iliyopo kisawani upande wa kusini ya
Malaysia, pia Singapore ni kitovu cha biashara ya kimataifa ikiwa na tamaduni
tofauti tofauti na tabia yake ya nchi ni aina ya Kitropiki. Singapore ina
wastani ya idadi ya watu wapatao 5.399 milioni kwa mujibu ya mwaka 2013, ikiwa
na GDP ya kiasi cha 297.9 bilioni fedha za marekani.
Denmark - $52,114
Denmark ni nchi ya Scandinavia ambayo ndani yake kuna
kisiwa cha Numerous na rasi ya Jutland. Wastani wa idadi ya watu ni sawa na
5.614 kwa mujibu wa takwimu ya mwaka 2013 na ikiwa na GDP YA 3335.9 bilioni
fedha za marekani. Uchumi wake wa kibiashara ni uchumi mchanganyiko, pia ina
rasilimali za asili kama mafuta na gesi yaliyopo bahari ya Kaskazini.
Ireland – $51,351
Jamhuri ya Ireland inamiliki pakubwa kisiwa cha
Ireland, nje ya pwani mwa Uingereza na Wales. Wastani wa watu waliopo kwenye
Jamhuri ya Ireland ni 4.595 milioni kwa takwimu za mwaka 2013 ikiwa na GDP ya
232.1 bilioni fedha za Marekani. Uchumi wake umeegamia kwa kiasi kikubwa huduma
za teknolojia, viwanda na uwekezaji.
Australia - $50,962
Australia ina sifa kuu mbili ya kwanza Australia
inatambulika kama nchi, nay a pili Australia ni bara linalojitegemea
imezungukwa na bahari ya Hindi na Pasifiki. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2013
ina wastani wa watu wapatao milioni 23.13 ikiwa na GDP ya 1.56 trilioni fedha za
Marekani. Uchumi wake ni uchumi wa soko mchanganyiko.
Iceland - $50,855
Iceland ni nchi ya kinodiki ikiwa na mandhari ya
kivolkano, chemic hemi ya maji moto. Kwa takwimu za mwaka 2013 idadi ya watu
nchini humo ilikuwa ni watu 323,002 ikiwa na GDP ya 12.3 bilioni fedha ya
Marekani. Uchumi wa Iceland ni mdogo ukiwa unategemea soko huru na
mchanganyiko.
Nchi tajiri duniani
Reviewed by info tza
on
12:43 PM
Rating:
Nice
ReplyDelete