Password (Nywila) ni nini?
Password ni neno la siri lenye muunganiko wa namba,
herufi, alama, ambayo inatumika kwenye mawasiliano ya mtu na mtu, mtu na
komputa au mtu na simu ili kuwa na udhibitisho mzuri kama ni yeye na kulinda
usiri wa muhusika.
Kuweka password kwenye komputa yako ni muhimu sana,
hasa kwa dunia ya sasa ambayo ukiangalia watu wengi wanapenda sana kutunza
nyaraka zao za siri kwenye komputa zao zinaweza zikawa nyaraka za ofisini pia.
Bila kuwa na password kwenye komputa yako inaweza kusababisha kudukuliwa kwa
nyaraka zako na kusambazwa kwa watu ambavyo ni hatari sana inaweza
kukusababishia hadi kufukuzwa kazi kama nyaraka za ofisi zitavuja na ikaja
kugundurika ni uzembe wako. Kwa misingi hiyo basi ni muhimu sana kuweka
password.
Mara baada ya kuwasha komputa yako. Windows itakutaka
uweke password kwa ajili ya akaunti yako. Kama utakuwa hapo awali uliitoa
password yako au ndo mwanzo umenunua komputa yako. Windows inakuruhusu kabisa
kuweka password uitakayo baada ya kuwa umewasha komputa yako kupitia User
account Features kwenye Control Panel.
Baada ya kuweka password yako, zima na washa komputa
yako au Bonyeza Windows icon + L kwa pamoja, windows itakuletea text bar ili
uweze kuweka password yako.
Kama ukiingiza password iliyokosewa, huwezi kupata
access ya files zako hakikisha unaweka password ambayo itakuwa ni rahisi sana
kwako kuikumbuka.
Kuweka password kwenye komputa yako kutakusaidia kuweza
kuzuia marafiki zako wasio wazuri ambao wanaweza wakaingia kwenye komputa yako
na kudukua nyaraka zako za siri na kuzisambaza.
Kuweka password kwenye komputa yako ni rahisi sana
fuata maelekezo haya rahisi sana.
- Bonyeza Start button, andika control panel kwenye Search Windows ili kuweza kufungua control Panel.
- Baada ya control panel kufunguka nenda na click User accounts. Click Continue kama User account control itataka udhibitishe kama unataka kufanya mabadiliko.
- Bonyeza jina la akaunti yako (Account name) kwenye listi, bonyeza Create a password.
- Ingiza password yako kwenye text bar, kasha bonyeza create password.
FAHAMU: Kuweka password nzuri unganisha namba, alama, herufi
iwe ndefu na rahisi kukumbuka. Usipende kutumia jina lako, la mpenzi wako,
ndugu zako, mwaka wa kuzaliwa au jina la kampuni au shule unayosoma na kufanyia
kazi.
Jinsi ya kuweka password kwenye komputa
Reviewed by info tza
on
11:48 PM
Rating:
No comments: