Pilau ni chakula kinachopendwa na watu wengi wa rika na
jinsia zote kutokana uzuri na utamu wake. Ila isipopikwa ipasavyo unaweza ukaiichukia
maisha yako yote usipende hata kunusa harufu yake.
Uandaaji wa pilau unahitaji umakini mkubwa kutokana na
aina mbalimbali za viungo vinavyotumika wakati wa maandalizi ya chakula yani
pilau. Ni vizuri kuchukulia kwa umakini mkubwa kipimo cha viungo utakavyoweka
kwenye pilau, la sivyo utafanya pilau yako ionekane mbaya na isiyo na radha
yoyote. Je, unapenda kujifunza kupika pilau vizuri kila mtu akaifurahia? Uko sehemu
sahihi, fuata haya maagizo rahisi sana.
Vitu vinavyotakiwa ili uweze kuandaa pilau
- Mchele : Mahitaji ya kiwango cha mchele kitatokana na ukubwa wa familia yako au wingi wa mchele wako unaoenda kuandaa. Hapa ntachukulia vikombe vitatu tu vya mchele kama mfano.
- Nyama: Mahitaji ya nyama pia yatatokana na ukubwa wa familia yako na wingi wa mchele pia. Kwa kila vikombe vitatu vya mchele andaa nusu kilo ya nyama ng’ombe, mbuzi au kuku.
- Viazi: Menya viazi vyako, kwa vikombe vitatu vya mchele. Weka viazi vitatu na nusu au vine sio vibaya ili isije viazi vikawa vingi sana zaidi ya mchele.
- Kitunguu maji: Andaa vitunguu maji kimoja na nusu au viwili sio vibaya.
- Kitunguu thomu: Andaa kitunguu thamu iliyosagwa vijiko viwili. Au andaa kitunguu swaumu ambayo haijasagwa kisha isagie kwenye vitunguu maji, tumia vipande vinne.
- Pilipili manga: Andaa nusu kijiko cha chai
- Pilau masala (Bizari ya pilau nzima): Pima nusu kijiko cha chai hakikisha hauzidishi la sivyo ikizidi itakifanya chakula chako kisiwe kizuri.
- Karafuu: Andaa karafuu nzima sita kama una Iliki pia unaweza kuchanganya iliki nzima sita.
- Mdarasini: Andaa vijiti vine au vitano vya mdarasini kasha vitangwe view kama unga unga.
- Chumvi: Andaa kiasi usiweke nyingi
- Mafuta ya kupikia: Andaa mafuta yako ya kupikia kutokana ni aina gani ya mafuta unapendelea zaidi.
Namna ya kutayarisha na kupika pilau nyama
- Roweka mchele wako kwa muda wa dakika tano kutegemea aina ya mchele kisha uoshe
- Kata kata nyama vipande vidogo vidogo au kutokana na mahitaji yako kisha osha kwa maji safi. Baada ya kuosha, weka kwenye sufuria kisha weka chumvi kiasi, pilipili iliyosagwa au kuchemshwa na mafuta, kitunguu thamu na tangawizi tiyari kwa kuchemsha.
- Ikiiva, angalia kama ina supu kisha epua weka kando
- Andaa sufuria lako jingine bandika kwenye jiko, kisha weka mafuta, vitunguu maji kanga mpaka vigeuke kuwa na rangi ya hudhurungi. Kisha weka kitunguu thomu na binzari kama unayo kisha kaanga kwa mda kidogo.
- Katakata viaze vipande vidogo vidogo kisha weka kwenye mchanganyiko, kaanga kwa mda wa dakika moja kisha weka vipande vyako vya nyama yenye supu. Acha ichemke kidogo.
- Weka mchele wako, kisha koroga uchanganyikane na viungo vyote na nyama. Kisha weka maji ya moto, koroga kidogo, kisha funika na punguza moto mpaka pale utakapoiva huku ukiwa unageuza geuza kidogo kidogo.
- Ukiwa tiyari, epua na pakua weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa na kachumbari yako ya aina yoyote, huku ukiwa na juice pempeni.
Jinsi ya kuandaa pilau
Reviewed by info tza
on
7:08 AM
Rating:
No comments: