Njia tano za kiasili za kuondoa chunusi
Baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la
chunusi linalowafanya waone wanatengwa au wananyanyapaliwa na wenzao wenye
imani potofu wakifananisha tatizo hilo na uchafu. Lakini hiyo halina ukweli kabisa.
Mara nyingine hasa tatizo la chunusi linatokana na kuwa
na mawazo na homoni ambazo ni vigumu sana kuzizuia.
Chunusi ni hali tu ya kawaida ya ngozi ambayo uwakumba
watu wengi rika zote kutokana na jinsi wanavyoendesha maisha yao.
Si tatizo
kubwa ambalo litamfaya mhusika awe na khali mbaya, ila itamfanya ijisikie
vibaya kutokana na mwonekano wake.
Kuna lotion na dawa nyingi sana kwenye maduka ya dawa
yanayotibu chunusi ila yanachukua mda mrefu sana. Lakini ukitumia njia za
kiasili zitakusaidia sana kupona haraka sana.
Hizi ni njia kumi za kiasili za kuondoa chunusi
Tumia juice ya limau
Hii ni njia mojawapo itakayokusaidia kutibu tatizo na
kuliondoa kabisa, inatokana na juice ya limau kuwa na vitamin C ambayo
inasaidia chunusi kukakuka haraka sana.
NB: Usitumie juisi limau ya madukani tumia limau
asilia. Fanya yafuatayo ili uweze kuona matokeo chanya.
Kata limau vipande viwili, kamulia juisi ya limau
kwenye chombo kisafi unaweza ukatumia bakuli, kikombe au chochote ulichonacho
ila kiwe kisafi.
Chukua kitambaa kisafi chovya juisi kidogo kidogo, paka
eneo lilio na chunusi kabla hujaenda kulala.
Dawa ya meno
Dawa ya meno unayoitumia kila siku kusafisha kinywa
chako, ni dawa tosha kabisa ya kuweza kuondoa chunusi kwenye ngozi
yako.
Hakikisha unatumia dawa nyeupe ya meno (white toothpaste) na sio gel
toothpaste.
Jinsi ya kufanya
Paka dawa ya meno sehemu ambayo imeathiriwa na chunusi
kabla hujaenda kulala, ili uwe na wakati mzuri wa kupumzika, ukiamka asubuhi
osha uso wako kwa maji safi. Kama huna kazi mchana rudia mara kwa mara kupaka
dawa, jitahidi ikae zaidi ya nusu saa.
Mvuke
Njia hii ni rahisi kuitumia mda wowote pale
unapojisikia. Mvuke utakusaidia kuzibua matundu ya ngozi yako yaliyoziba na
kufanya ngozi yako ipata kupumua vizuri.
Itasaidia kuondoa mafuta, uchafu na
bakteria waliojificha au kubanwa kwenye matundu, usipowaondoa kwenye hayo
matundu itakusababishia chunusi.
Njia za kufanya
Chemsha maji yachemke, epua weka kwenye chombo chako
ulichoandaa mfano bakuli kubwa, inamia hicho chombo chako ukiruhusu mvuke uje
moja kwa moja usoni mwako kwa dakika chache tu.
Kisha safisha uso wako kwa maji ya uvuguvuvugu, chukua
kitambaa kisafi cheupe kama utaweza, jikaushe na jiapake mafuta(free moisture
oil).
Asali
Asali ni tiba ya magonjwa mengi, chunusi ni mojawapo
fanya yafuatayo kutumia asali kutibu chnusi
- Weka asali yako kwenye bakuli
- Chukua pamba zungusha kwenye asali na weka moja kwa moja sehemu iliyoathirika, acha ikae kw mda kama dakika 15,
- Osha kwa maji ya uvuguvuvugu.
- Fanya hivyo angalau mara tatu kwa siku
Tango
Tango linazalisha potassium na vitamin A, C na E ambayo
inasaidia kupoza ngozi yako.
Jinsi ya kutumia
Kata tango vipande vidogovidogo, chukua vipande vitatu
tumbukiza ndani ya maji vikae kwa saa moja kwa ajili ya kuruhusu virutubisho
vyote vile visambae kwenye maji.
Chuja maji yako kunywa au tumia hayo maji kuosha uso
wako.
Papai
Njia za kufanya
Chukua vipande vidogo vidogo vya papai saga, paka
sehemu iliyoathirika subiri kwa zaidi ya dakika 10 kabla ya kusafisha.
Au chukua vidogo vidogo vya papai changanya na asali
kidogo. Weka sehemu iliyoathirika na usugue taratibu, subiri ikauke then itoe.
Njia za kuondoa chunusi
Reviewed by info tza
on
5:09 AM
Rating:
No comments: