Qatar imeapa kwamba haitasalimu amri katika mzozo wake kuhusu sera yake ya kigeni na nchi nyingine za Kiarabu kutokana na ukaribu uliopo kati ya Qatar na kundi la Undugu wa Kiislamu la nchini Misri lililokuwa nchini ya Raisi aliyeng'olewa madarakani Mohammed Morsi pamoja na nchi ya Iran ambayo ni hasimu mkubwa wa nchi za Saudi Arabia, Falme za Kiaarabu.
Nchi hizo tano za Ghuba zilizoafiki vikwazo dhidi ya Qatar zinaituhumu Qatar kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi likiwemo kundi la dora ya kiislamu linalopigana Iraq na Syria na makundi yenye msimamo mkali.
Waziri wa mambo ya nje wa Qatar Sheikh Mohammed bin Abdulrahman al-Thani amesema anaunga mkono zaidi kutumiwa kwa demokrasia kutatua mzozo huo na kwamba hakuwezi kuwa na suluhu inayoweza kupatikana kupitia nguvu za kijeshi, ameambia Reuters.
Qatar imepuuzilia mbali tuhuma hizo kwamba inaunga mkono makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali.
Qatar yangaka kuhusu mzozo wake na nchi baadhi za Ghuba
Reviewed by info tza
on
12:42 AM
Rating:
No comments: