Bunge la Japan limeidhinisha sheria itakayomuwezesha Mfalme wa nchi hiyo Akihito kuondoka madarakani, jambo ambalo litakuwa la kwanza kwa mfalme kung'atuka nchini humo kwa zaidi ya miaka mia mbili.
Zoezi la upigaji kura katika bunge la juu, limeoneshwa moja kwa moja na Televisheni.
Sheria hiyo mpya ilianza kupitishwa na bunge la chini wiki iliyopita.
Mfalme Akihito mwenye umri wa miaka 83 aliishangaza nchi hiyo, mwaka uliopita kwa kuelezea nia yake ya kung'atuka, kutokana na afya yake na umri.
Mwana wa Mfalme Naruhito anatarajiwa kushika nafasi hiyo.
#BBC
Bunge nchini Japan laidhinisha Mfalme kung'atuka
Reviewed by info tza
on
12:26 AM
Rating:
No comments: