Helikopta hutumika zaidi hasa katika utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu, vitani na kuokoa watu ikiwa wametekwa na vikundi vya kigaidi au wamezingiliwa na hatari kama mafuriko, maporomoko. Helokopita za kwanza kabisa zilionekana kipindi cha vita ya pili ya dunia, vita ya Vietnam na Marekani. Ila kutokana na ukuaji wa Teknolojia hivi sasa kuna helokopita za kisasa kabisa ambazo hutumika zaidi kwa shughuli za vita, hapa nimekuletea helekopita tano hatari sana duniani.
AH-64D Apache Long Bow
Hii ni helikopta yenye nguvu sana aina ya boeing AH-64
Apache Attack imetengenezwa mahususi kwa jeshi la marekani kwa ajili ya kufanya
kazi maalumu bila kujali kama ni usiku, mchana au ikiwa hali ya hewa ni mbaya
kiasi gani na imetumika sana hasa sehemu za guba. Ina uwezo wa kubeba makombora
16 ya aina ya AGM-114 Hellfire.
Kamov KA-50/KA-52
Hii ni helikopta ndogo, yenye kasi kubwa sana ya jeshi
la Urusi yenye kiti kimoja tu kwa jili ya rubani tu ikiwa kazi yake kubwa ni kufanya
mashambulizi kwa jina jingine inaitwa “Black Shark” iliundwa miaka ya 1980s
lakini ilianza kutumiwa na jeshi la Urusi mnamo mwaka 1995. Ina uwezo wa kubeba
makombora 24 ya aina ya VIKHR pia inaweza ikabeba makombora ya anga ya aina ya
AA-11/R-73 Archer.
MI-28H Havoc (Russia)
Ni helikopta ya jeshi la Urusi, ina uwezo wa kubeba
watu wawili pia ina uwezo wa kufanya mashambulizi mda wowote bila kujali hali
ya hewa iliyopo iwe mchana au usiku.
Eurocopter Tiger
Ni aina ya helikopta ambayo mission yake kubwa ni
kushambulia, imetengenezwa na Eurocopter inapatikana katika nchi ya Ujerumani
ikifahamika zaidi kwa jina la Tiger na katika nchi za Ufaransa na Hispania
inafahamika zaidi kwa jina la Tigre.
AH-1Z Viper
Inatumika zaidi kwenye shughuli mbalimbali kama za
uokoaji, na kushambulia pia. Ilitengenezwa kwa ajili ya Jeshi la Marekani
ikijulikana zaidi kama “Zulu Cobra”.
Hapa nimekusogezea helikopta tano bora duniani za kivita
Reviewed by info tza
on
2:39 PM
Rating:
No comments: