Tanzania yaadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara 2017


Tanzania imeadhimisha miaka 56 ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania bara)  baada ya kupata uhuru kutoka koloni la mwingereza disemba 9 mwaka 1961. Harakati zote za kupata uhuru zilikuwa zikiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere raisi wa awamu ya kwanza wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Kwenye maadhimisho hayo vikosi vya ulinzi na usalama vilionesha mbinu mbali mbali za kivita ikiwa pamoja na Gwaride la jeshi na onesho la makomando wa jeshi la wananchi JWTZ.  Pia raisi Magufuli ameweza kutoa msamaha kwa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na kuagiza kuachiliwa kwa mwanamuziki maarufi wa dansi Nguza Vicky maarufu kama babu Seya na mwanae wa kiume. 

Kuangalia video ya maadhimisho ya uhuru 


Tanzania yaadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara 2017 Tanzania yaadhimisha miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara 2017 Reviewed by info tza on 12:05 PM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.