Akiwasilisha bajeti ya serikali ya mwaka 2017/2018 waziri wa fedha na mipango Mheshimiwa Phillip Mpango amesema serikali haitaruhusu usafarishaji wa madini wa moja kwa moja kutoka mgodini na kupelekwa nje ya nchi.
Badala yake kutakuwepo na viwanja maalum vya kimataifa katika bandari, migodini na madini hayo yatathibitishwa na kupewa kibali maalumu kabla ya kusafirishwa nje. Ambapo kibali hicho kitatozwa ada ya asilimia moja ya thamani ya madini hayo.
Amesema serikali itatangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa ada hiyo.
Serikali yazuia usafirishaji wa madini wa moja kwa moja kutoka mgodini
Reviewed by info tza
on
1:17 AM
Rating:
No comments: