Korea kaskazini imerusha makombora kadha ya kushambulia meli mashariki mwa pwani yake hii leo alhamisi, kwa mujibu wa Korea Kusini.
Mamlaka zilisema kwa makombora hayo yaliyorushwa Alhamisi asubuhi karibu na mji wa Wonsan yalikuwa ni ya masafa mafupi.Makombora hayo yaliruka umbali wa kilomita 200 ambayo ni sawa na miles 124 kabla ya kuanguka baharini.
Katika majaribio 10 ya kurusha makombora, Korea Kaskazini imefanikiwa kurusha makombora 16 na jaribio la leo lilikuwa la nne tangu Raisi mpya wa nchi ya Korea Kusini Moon Jae alipoingia madarakani mwezi wa tano mwaka huu.
Korea kaskazini yarusha kombora la kushambulia meli
Reviewed by info tza
on
12:38 AM
Rating:
No comments: