Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA Nchini Somali na Kuwaua 57



 Wanajeshi wa Kenya wakiwa kwenye gari lao la kijeshi

Kundi la al-shabab nchini Somalia limedai wapiganaji wake wameishambulia kambi ya kijeshi ya Kenya iliyopo nchini Somalia chini ya kivuli cha AMISOM

Wanamgambo hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi wa nchi ya Kenya walioko kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka na nchi ya Kenya

"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters. 

Msemaji huyo wa kundi la Al-shabab amedai wamewaua wanajeshi wa Kenya hamsini na saba, na kutwaa magari na silaha walizokuwa nazo wanajeshi hao wa Kenya. 

Akizungumza na kituo cha Reuters Kanali Paul Njuguna amesema : "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa." 

Kundi la kiislamu lenye itikadi kali la al-shabab limekuwa likipigana dhidi ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa zikiwemo nchi za magharibi. 
Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA Nchini Somali na Kuwaua 57 Al-Shabab Washambulia kambi ya Wanajeshi wa KENYA Nchini Somali na Kuwaua 57 Reviewed by info tza on 2:50 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.